KUMBE

KIKUNDI CHA UTALII MBEYA


Miradi yetu
Katiba ya KUMBE
Wanachama
Guestbook

 
UWAZI
Search

ELIMU NA UTALII NCHINI TANZANIA

Karibu jiunge katika Kikundi cha Utalii Mbeya (KUMBE) na changia katika maendeleo ya utalii na elimu.

BONGO CAMPING

     Wahusika wa mradi wetu wa kwanza uitwao Bongo Camping ni vyama viwili rafiki: sisi wanachama wa Kikundi cha Utalii Mbeya (KUMBE), Tanzania, na Bongo Development Tourism (BDT), Denmark. Mradi wetu wa maendeleo tumeutayarisha baada ya kujiuliza suali lifuatalo, je italeta faida gani kuunganisha fani mbili za utalii na elimu?

     Kwanza tukiangalia sura za fani za utalii na elimu kwa pamoja tunafikia mahali panapolingana: Pande zote mbili utalii na elimu zinahusika na watu wanaojifunza mambo mapya wakiwa nje ya biashara za dunia: wanafunzi hukaa kusoma, kuandika na kuhesabu; watalii hutembea kuchunguliza mazingira. Tukiachana na starehe ile wanaoihitaji watalii, shughuli zao pia ni kuweka mambo mapya akilini waone maendeleo ya ujuzi wa binafsi. Vilevile wanafunzi wanatakiwa kuweka mambo mapya akilini ndio wakati huu tunauita wakati wa kutafuta ”funguo ya maisha”.      

     Siku hizi bado tunao uwezo wa kulazimisha utalii uwe kama mchango katika maendeleo mengine nchini ilimradi tunaamua mbinu za utalii zitumike kushughulikia mambo yanayoelimisha wananchi. Tena hali hiyo ingetupa sisi wananchi nafasi kubwa za kuzidi kulisukuma taifa letu liwe katikati ya dunia ya kimataifa. Ukizingatia maendeleo ya kisasa, ni mambo mengi tu ambayo yanakuwa ni ya kimataifa – mawasiliano ya biashara, teknolojia mpya, siasa ya nje n.k. Mbinu zinazotumika katika fani ya utalii zingetuwezesha sisi watanzania tujifunze zaidi utumiaji bora wa sehemu hizo za kimataifa. Kuiendeleza mbinu ya mtandao; kujifunza utumiaji bora wa teknolojia mpya; kubadilishana ujuzi wa siasa na wageni wanaolijali taifa letu; zote ni misingi ya mabadiliko mema yanayoweza kuzidi kuliweka taifa letu katika ramani ya nchi yenye maendeleo barani Afrika.

     Mradi wetu wa maendeleo, uitwao ”Bongo Camping” – ambao wahusika wake wa nje wote wamewahi kutalii nchini Tanzania – unaonyesha kwamba ikiwa sisi watanzania tunaichukua nafasi ya kuwatia moyo watalii washirikiane au kuchangia katika utalii wa kimaendeleo, ndio tutaziboresha sehemu mbalimbali za elimu ambazo zinafaa kuitwa sehemu za kimataifa. Kwa mfano utalii jinsi unavyolazimisha utumiaji wa mtandao na wa lugha za kimataifa (kiingereza, kifaransa, na lugha zingine za kiafrika) hiyo ndiyo ni nafasi ya kuboresha elimu za kisasa nchini kwetu. Utalii utazalisha matunda mengi zaidi nchini kwetu ikiwa tunaifanya fani hiyo iwe sehemu ya kutekeleza mbinu za mawasiliano na lugha, ndio itakuwa na faida kubwa katika pande zote mbili utalii na elimu. Kusema kwa uwazi, utalii utakuwa ni msingi wa hela na mbinu zitakazotumika upande wa elimu, na wote wageni na wenyeji watazidi kutambua hivyo ndivyo jinsi bora ya kujiunga katika utalii wa kimaendeleo.

 



This is a border element

ONA PICHA NYINGI ZA TUKUYU NA MBEYA, GONGA HAPA


KARIBU MBEYA - KARIBU TUKUYU




Top top uwazi.com, Bongo Dev. Tourism, Ukerewe Turist Ass., Lønindikator - tjek din løn